Manchester United inaweza kuwauza Jadon Sancho na Donny van de Beek kwenda Juventus kwa pauni milioni 26 pekee.

Gazeti la The Sun limeripoti kuwa wawili hao hawana mustakabali wa kuishi Old Trafford na wataachiliwa kwa bei nafuu haraka iwezekanavyo.
Ndugu mteja tembelea duka la ubashiri la Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.
Jim Ratcliffe anatazamiwa kukamilisha ununuzi wake wa 25% ya klabu na moja ya hatua zake za kwanza itakuwa kukiboresha kikosi. Wanaotarajia kutwaa taji la Serie A Milan wanaweza kuwa miongoni mwa watakaofaidika huku wakitafuta kuendeleza changamoto yao.
Sancho hajacheza United tangu alipotofautiana hadharani na kocha wake Erik ten Hag baada ya kushindwa na Arsenal mnamo Septemba.
Ten Hag alimshutumu winga huyo kwa kutofanya mazoezi ya kutosha ili kuchaguliwa, tuhuma ambayo mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza baadaye aliita “uongo”.
Na kukataa kwake kuomba msamaha kunamaanisha kuwa amefungiwa. Uchezaji wa Van de Beek Old Trafford haujafanikiwa, huku Mholanzi huyo akicheza mechi mbili pekee kufikia sasa msimu huu.
Vilevile meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.
Amefunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao katika mechi 62 tangu asajiliwe mwaka 2020 na huenda hatma yake pia ikawa mbali na Manchester.