Kobbie Mainoo Kukipiga Dhidi ya Everton leo

Kiungo kinda wa klabu ya Manchester United Kobbie Mainoo atakipiga leo dhidi ya klabu ya Everton akiwa moja ya wachezaji wanaoanza katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo.

Kobbie Mainoo ambaye amerejea kutoka kwenye majeraha mwezi mmoja uliopita hakufanikiwa kupata nafasi katika timu ya wakubwa ya klabu hiyo, Lakini leo atacheza mchezo wake wa kwanza tangu atokea kwenye majeraha.kobbie mainooMchezo wa leo kwa kijana huyo mwenye miaka 18 tu hautakua mchezo wake wa kwanza tangu atoke kwenye majeraha, Bali utakua mchezo wake wa kwanza kuanza katika ligi kuu ya Uingereza.

Kinda huyo hakuwahi kufanikiwa kuanza katika mchezo wowote wa Man United wa ligi kuu ya Uingereza, Lakini leo ataanza na kocha Erik Ten Hag amesema kijana huyo yuko tayari kucheza baada ya kutoka kwenye majeraha kwakua ameshacheza michezo kadhaa akiwa na timu ya vijana.kobbie mainooKiungo Kobbie Mainoo amekua akionesha ubora mkubwa sana katika timu ya vijana ya klabu hiyo, Lakini pia kwenye michezo ya kujiandaa na msimu ya Man United jambo ambalo limefanya kocha Ten Hag amuamini kijana huyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.