Aston Villa Waichapa Tottenham

Klabu ya Aston Villa imefanikiwa kuifunga klabu ya Tottenham Hotspurs kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza ambao umepigwa jioni ya leo.

Aston Villa chini ya kocha Unai Emery imeendeleza ubora wake leo wakiwa ugenini na kuweza kuchomoza na ushindi mbele ya klabu ya Tottenham ambao walianza vizuri ligi kuu ya Uingereza.aston villaKlabu ya Tottenham ndio walikua wakwanza kupata bao kupitia kwa kiungo Giovani Lo Celso kabla ya beki Pau Torres kuisawazishia Villa kabla ya kwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama ambavyo kipindi cha kwanza kilivyokua na timu zote zikiendelea kutafuta bao la pili ili kua mbele, Lakini ni Aston Villa waliofanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Ollie Watkins na mchezo huo kumalizika kwa Villa kuibuka na ushindi.aston villaVijana wa kocha Unai Emery baada ya matokeo ya ushindi ya leo dhidi ya Tottenham Hotspurs yamewavusha moja kwa moja mpaka nafasi ya nne kwneye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza wakiwa na alama zao 28, Huku wakilingana alama na Liverpool tofauti ikiwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.