Liverpool Yaondoka na Alama Tatu Molineux

Klabu ya Liverpool imefanikiwa kuibuka na alama tatu muhimu katika dimba la Molineux ambapo walikipiga dhidi ya klabu ya Wolves ambayo walikua katika uwanja wao wa nyumbani.

Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Wolves ambapo magoli yote ya Majogoo waliyapata katika kipindi cha pili baada ya kutanguliwa kufungwa katika kipindi cha kwanza.liverpoolKlabu ya Wolves walifanikiwa kupata mapema kabisa kipindi cha kwanza dakika ya 7 ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji Hwang Hee Chan na kuwapa uongozi Mbwa mwitu hao mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika walikua wanaongoza kwa bao moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Majogoo wa Anfield walikuja kwa kasi na kufanikiwa kusawazisha bao kupitia kwa Coady Gapko mnamo dakika ya 55 ya mchezo kabla ya beki Robertson kuongeza bao la pili na kuwapa uongozi Majogoo.liverpoolKlabu ya Liverpool ilipata bao la tatu kupitia shuti lililopigwa na kiungo Harvey Elliot na beki Bueno kujifunga na kuwafanya majogoo kuhitimisha ushindi wao katika dimba la Molineux, Huku wakifikisha jumla ya alama 13 katika michezo mitano waliyocheza na wakiwa kileleni mpaka sasa.

Acha ujumbe