Makocha Walioiongoza United

Klabu ya United imeweza kuongozwa na makocha wa pekee na wenye historia kubwa kikosini hapo. Kati ya idadi hiyo ya makocha wapo walioondoka patupu bila kuacha mataji ya aina yoyote ndani ya klabu hiyo na wengine wakifanikiwa kutwaa mataji. Leo tutakuletea baadhi ya makocha waliopita klabuni hapo kwa vipindi tofauti.

Jose Mourinho, baada ya kuhudumu na Chelsea kwa kipindi kirefu na kuwaachia mafanikio makubwa, kocha huyo aliweza kukubali kuinoa United Mei, 27 2016 katika mkataba aliosanishwa na klabu hiyo. Aliweza kupokea kijiti kilichorushwa na Van Gaal baada ya kushindwa kupata kile kinachotakiwa na uongozi wa klabu.

Louis Van Gaal, aliweza kuiongoza klabu hiyo kwa kipindi kifupi na baada ya kushindwa kuendana na kasi ya maendeleo ambayo klabu iliwekeza kwake wakaamua kuachana naye kusudi likiwa ni kupata mtu atakayekipatia mataji zaidi kikosi hicho. Akiwa na klabu hiyo alifanikiwa kuchomoza na taji la FA aliloshinda kutoka kwa Crystal Palace.

David Moyes, alibahatika kushinda Ngao ya Jamii pekee ndani ya kikosi hicho jambo ambalo lilionekana kama linahitaji nguvu ya ziada kwa kocha huyo kushinda mataji mengine zaidi kutokana na mfumo wake. Aliweza kutua kwa kasi kikosini hapo lakini akashindwa kufikia malengo ya kimkataba kati ya wawili hao.

Alex Ferguson, ni kati ya watu ambao wapo kwenye akili na kichwa cha yeyote anayependa soka zuri. Ni mtu ambaye falsafa zake kisoka ni zenye upekee mkubwa sana. Baadhi tu ya mataji aliyoyakusanya kikosini hapo ni kama: 13 ya ligi, matano [5] ya FA, manne [4] ya kombe la ligi, 10 ya ngao ya hisani ya FA, mawili ya klabu bingwa Ulaya, moja [1] ya kombe la washindi wa klabu bingwa Ulaya, moja [1] la super cup ya klabu bingwa Ulaya, kombe la mabara ngazi ya klabu [1], kombe la dunia la FIFA ngazi ya klabu. Ni mafanikio ambayo hayawezi kuvunjwa kabisa.

Ron Atkinson, raia huyo wa Uingereza aliiongoza United miaka ya 1981 hadi 1986. Alijitahidi kuipa angalau mataji klabu hiyo mbele ya klabu nyingine kubwa. Aliwapa ushindi wa vikombe viwili vya FA na kombe moja la ngao ya hisani kwa kipindi hicho cha mafanikio kabla ya kuachia nafasi hiyo mbele ya Sir. Alex.

Dave Sexton, aliiongoza kwa mafanikio finyu klabu hiyo baada ya kushinda kombe moja pekee la ngao ya jamii mwaka 1977; yaani mapema tu alipotua klabuni hapo. Kutokana na mwenendo huo aliweza kupoteza nafasi yake hiyo kama kocha na kuwaachia wengine waliokuja kuleta changamoto zaidi.

Hao ni baadhi tu ya makocha waliojenga msingi wa United inayoonekana leo kuwa klabu kubwa. Hawawezi kusahaulika kwa makubwa hayo waliyoyafanya klabuni hapo. Na kwa hakika waliacha msingi mzuri ambao kila mmoja anajivunia kuona ndani ya klabu hiyo. Kwa sasa mikoba iko chini ya Ole Gunnar.

2 Komentara

    Hongera kwa waliofanikiwa

    Jibu

    Daah sikujua kama kocha Jose alipitia Manchester united bila kuweka historia yoyote nimejua sasa

    Jibu

Acha ujumbe