Man United Kuachana na Pogba 2022?

Ukipenda, hii wiki unaweza kuipa jina la ‘Wiki ya Man United’. Kila uchwao, The Red Devils wapo midomoni mwa watu. Hakika, hii ni klabu ya dunia.

Toka wapoteze michezo 2 ya EPL mfululizo, kwa vipigo vikali. United imekuwa ikitamba kwenye vyombo vya habari na miongoni mwa wadau wa soka. Kumtimua Ole Gunnar Solskjaer, nani kuchukua kibarua cha kuongoza timu? Nani mchawi – kocha, wachezaji au uongozi?

Ukigusia upande wa wachezaji, majina mawili yanateka ulimwengu wa soka. Cristiano Ronaldo na Paul Pogba. Wakati United ikitaabika, wapo wanaomsema vibaya CR7 na Pogba miongoni mwa wachezaji wakubwa wa Man United. Michango yao ni ipi? Viwango vyao vinaendana na kile kinachotokea uwanjani wakiwa ndani ya uzi mwekundu?

Yote 9, 10 ni suala la mkataba wa Paul Pogba. Ni takribani miezi 8 sasa, hatma ya mchezaji huyo haijulikani. Mchakato umekua wa kuanza na kusimama mara kwa mara. Ifikapo Januari, kwa hali ilivyo sasa hivi, Pogba yupo huru kuzungumza na klabu yeyote nje ya EPL.

Inasemekana kuwa, Man United wamejiandaa na maisha bila ya Pogba. Hii inamaana kuwa, wapo tayari mchezaji huyo kuondoka klabuni hapo muda wake utakapokwisha. Japokuwa, The Red Devils hawaoni sababu yeyote ya kumuuza Pogba mwezi januari. Badala yake, watamuacha mchezaji huyo aondoke bure mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mchezaji aliyesajiliwa kwa dau kubwa kwenye historia ya United (£89M), inawezekana akaondoka kama mchezaji huru ifikapo 2022?


MCHONGO WA PESA NA CIRCUS FEVER

Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.