Manchester City Waweka 90 kwa Rice

Klabu ya Manchester City wamefanikiwa kupeleka ofa kwa klabu ya West Ham kwajili ya kiungo wa klabu hiyo raia wa kimataifa wa Uingereza Declan Rice.

Manchester City wamepeleka kiasi cha puandi milioni 90 kwa klabu ya West Ham wakihitaji saini ya kiungo Declan Rice ambaye amekua akiwindwa na klabu ya Arsenal, Lakini City wanaonekana kama wako na imani kubwa ya kumpata kijana huyo.Manchester CityPaundi milioni 100 ndio dau ambalo linaweza kumtoa Declan Rice ndani ya klabu ya West Ham United huku vilabu vyote viwili yaani Man City na Arsenal wote wakiwa wametoa ofa ya paundi milioni 90 jambo ambalo linasubiriwa ni klabu gani itaweza kumtwaa mchezaji huyo.

Manchester City walionesha kumuhitaji kiungo Declan Rice wiki moja nyuma lakini hawakufanikiwa kuweka ofa yao mezani, Lakini jana matajiri hao kutoka jijini Manchester wameweka ofa ya kwanza kwa klabu ya West Ham ya paundi milioni 90.Manchester CityArsenal wao bado wanaamini wanaweza kumpata mchezaji huyo kwani wao ndio walikua wanaongoza mbio za kumpata Declan Rice lakini kuingia kwa Manchester City kwenye mbio hizo inakua tishio kwa washika mitutu hao wa London kwani mtanange unaenda kua mkali sana.

Acha ujumbe