Klabu ya Manchester City imetawala kwenye kikosi cha wachezaji bora wa ligi ya mabingwa ulaya msimu huu baada ya kufanikiwa kuingiza wachezaji saba.
Kikosi cha Manchester City ambacho ndio kimetwaa ubingwa wa ulaya msimu huu wachezaji wake wamekua kwenye ubora mkubwa na ndio sababu wamefanikiwa kuingiza wachezaji saba kwenye kikosi bora cha ligi ya mabingwa ulaya msimu huu.
Wachezaji wa mabingwa hao wa ulaya walioingia kwenye kikosi bora cha ulaya ni pamoja na beki Kyle Walker,Reuben Dias,John Stones, Kevin de Bruyne, Rodri,Bernardo Silva, na Earling Haaland huku timu zingine zikichangia wachezaji wanne waliobakia.
Ukiachana na wachezaji wa klabu ya Manchester City ambao wamekua na msimu bora na kutawala orodha ya kikosi bora cha msimu, Lakini wachezaji wengine waliongia kwenye kikosi ni golikipa Thibaut Courtois, mabeki Federico Dimarco na Bastoni kutoka Inter Milan, pamoja na winga wa Real Madrid Vinicius Jr.
Manchester City ni wazi wamestahili kutawala orodha ya kikosi bora cha msimu kwenye ligi ya mabingwa ulaya na hiyo ni kutokana na wachezaji wa klabu hiyo kua kwenye viwango vya juu ambapo wamechangia klabu yao kutwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo.

