Klabu ya Tottenham Hotspurs imeripotiwa kumfukuzia winga wa klabu ya Manchester United Jadon Sancho katika dirisha hili la usajili ili kuboresha kikosi chao.

Sancho ambaye alijiunga na klabu ya Manchester United mwaka 2021 anahitajika na klabu hiyo kutoka kaskazini mwa jiji la London ili kuhakikisha warudi kwenye ubora wao baada ya kua na msimu mbovu mwaka 2022/23.SanchoKlabu ya Manchester United inaripotiwa kuhitaji kiasi cha Euro milioni 60 ili kumuachia winga huyo wa kimataifa wa Uingereza, Kama Tottenham watakubali kutoa kiasi hicho cha pesa ni wazi mchezaji huyo ataelekea Spurs msimu ujao.

Jadon Sancho tangu ajiunge ndani ya klabu ya Manchester United amekua na kiwango cha kusuasua kitu ambacho kimefanya klabu hiyo kufikiria kumuuza kwani ni msimu wa pili sasa hajafnikiwa kuonesha ubora ambao alikua nao ndani ya Borussia Dortmund.SanchoKlabu ya Manchester United ina mpango wa kuondoa wachezaji kadhaa klabuni hapo kuelekea dirisha hili kubwa ili waweze kusajili wachezaji wengine wenye ubora mkubwa, Huku Jadon Sancho akiwa kwenye orodha hiyo hivo klabu ambayo itafika bei wanayoitaka United mchezaji huyo atauzwa Spurs nao wakiwa ndio wako mstari wa mbele.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa