Klabu ya Manchester United ipo kwenye mazingira mazuri ya kumchukua golikipa namba moja wa klabu ya Fc Porto pamoja na timu ya taifa ya Ureno Diogo Costa ambapo inataarifiwa kipa huyo ataondoka klabuni hapo.
Manchester United imekua ikimfatlia kipa huyo wa kimataifa wa Ureno kwa muda mrefu sasa, Golikipa huyo anamvutia zaidi kocha wa timu hiyo Erik Ten Hag na anatazamiwa kua mbadala wa muda mrefu wa golikipa mkongwe klabuni hapo David de Gea raia wa kimataifa wa Hispania.
Golikipa Diogo Costa kupitia watu wake wa karibu inaelezwa kipa huyo anajiandaa kuondoka ndani ya Porto majira haya ya joto, Huku akili yake ni kujiunga na Man United ambao wamekua wakimfukuzia kwa muda licha ya vilabu kama Newcastle na Tottenham kuonesha kuhitaji huduma yake.
Klabu ya Manchester United chini ya kocha Erik Ten Hag wanahitaji golikipa ambae anaweza kucheza kuanzia nyuma na mwenye utulivu na mpira mguuni, Kwani mfumo wa kocha huyo unahitaji golikipa wa aina ambapo mpaka sasa David de Gea anaonekana bado sio mtu sahihi licha ya ubora wake wa kuzuia mashuti.
Kocha wa Manchester United wiki moja nyuma aliweka wazi kua klabu inahitaji golikipa mpya wa kuweza kupeana changamoto na David de Gea, Huku akiweka wazi mpira wa kisasa unahitaji golikipa ambaye anaweza kucheza mpira kuanzia nyuma ili kuepuka presha ya wapinzani.

