Klabu ya Manchester United baada ya kuachana na mkurugenzi wake wa michezo raia wa kimataifa wa Uingereza Dan Ashowrth inaelezwa kwasasa wanamfukuzia mkurugenzi wa michezo wa Atletico Madrid ya nchini Hispania.
Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Atletico Madrid kwasasa ni raia wa kimataifa wa Italia ambaye anaitwa Andrea Berta ambaye ana zaidi ya miaka 10 ndani ya klabu hiyo nchini Hispania, Kwani alijiunga na klabu hiyo ya nchini Hispania mwaka 2013 mwezi Mei na ameendelea kusalia klabuni hapo mpaka sasa akiwa amefanya kazi kubwa sana akishirikiana na kocha Diego Simeone.