Manchester United Kumtema Greenwood kisa Mashabiki

Klabu ya Manchester United inaelezwa inatarajia kumtema mchezaji Mason Greenwood kutokana upinzani mkali kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo wasiotaka mchezaji huyo arejee.

Manchester United walitoa taarifa ya umma siku ya Alhamisi ambayo ilionesha wanakaribia kutoa maamuzi juu ya mchezaji huyo, Lakini mashabiki wengi waliona kama klabu hiyo imepanga kumrudisha klabuni hapo ambapo ndipo gumzo lilipoibuka na kundi kubwa likionekana kumkataa.manchester unitedTaarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zilikua zinaeleza kua mkurugenzi wa klabu hiyo alishafanya maamuzi ya kuamua kumrejesha Greenwood kikosini, Lakini baada ya mashabiki wa klabu hiyo kuonekana kuwa wakali klabu hiyo imeamua kusitisha klabu hiyo.

Klabu ya Man United walikiri kua jambo la Mason Greenwood limekua moja ya mambo magumu sana kutolea uamuzi kwa watu wote waliokua ndani ya klabu hiyo na hiyo ni kutokana na mchezaji huyo kua zao la klabu hiyo.manchester unitedManchester United inaelezwa imefikia uamuzi wa kupiga chini suala la kumrudisha Mason Greenwood klabuni hapo licha ya kuhitaji kumrudisha mchezaji huyo, Lakini mapokeo hasi ya mashabiki wa klabu hiyo ndio yamesababisha klabu hiyo kuachana na mpango huo.

Acha ujumbe