Klabu ya Manchester United inaelezwa itaingia sokoni kutafuta beki wa kushoto ambaye atakuja kusaidiana kazi na beki wa kimataifa wa Uingereza klabuni hapo Luke Shaw.
Manchester United inaelezwa wanapanga maboresho makubwa ya kikosi chao na eneo la beki wa kushoto ni moja ya eneo ambalo wanalitazamia kuliboresha, Kwani beki Luke Shaw mara nyingi amekua akisumbuliwa na majeraha.Mazungumzo yanaendelea ndani ya bodi ya timu ili kuandaa orordha ndogo ya mabeki wa kushoto ambao watawafatilia kwa karibu kuelekea dirisha kubwa, Kwani mabosi wa klabu hiyo wamedhamiria kwelikweli kukiboresha kikosi hicho.
Moja ya mabeki wa kushoto ambao wamekua wakizungumzwa sana kutakiwa na klabu ya Man United ni beki wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga ndani ya klabu ya Ac Milan Theo Hernandez, Kwani amekua kwenye kiwango bora sana ndani ya klabu ya Milan na amekua moja ya mabeki wa kushoto wenye ubora mkubwa sana barani ulaya.Mabeki wengine ambao wanafanya vizuri kwasasa barani ulaya ni pamoja Alex Grimaldo anayekipiga pale Bayern Leverkusen, Federico Dimarco anayekipiga klabu ya Inter Milan nao wanahusishwa sana na klabu ya Manchester United, Huku ikionekana ni wachezaji ambao wanaweza kua watu sahihi wa kuvaa viatu vya Luke Shaw.