Baada ya kuambulia suluhu katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Galatasaray, Jana Manchester United wameendelea walipoishia kwani wamepoteza mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Newcastle United.
Manchester United jana wamepoteza mchezo wa sita wa ligi kuu ya Uingereza jana, Hii imekuja baada ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Newcastle United katika dimba la St. James Park usiku wa jana.Man United jana walionekana klabu dhaifu sana katika mchezo dhidi ya Newcastle, Huku ikionekana ni mchezo ambao klabu hiyo imecheza vibaya zaidi msimu huu kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Mashetani Wekundu licha ya kupoteza mchezo wa jana kwa bao moja kwa bila lakini walionekana kutawaliwa kwa kiasi kikubwa na Newcastle, Huku wakimaliza kwa kupiga shuti moja tu lililolenga lango katika mchezo huo.Mashabiki wa Manchester United wameanza kuonesha kutoridhishwa na muenendo wa kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag, Huku wengine wakiona kama kocha huyo ameshindwa kufanya kile kilichotarajiwa licha ya kufanya usajili mkubwa.