Barcelona Dhidi ya Atletico Madrid Moto Utawaka Leo

Leo pale nchini Hispania moto utawaka sana kwenye ligi kuu nchini humo klabu ya Barcelona watakua nyumbani kuwakaribisha klabu ya Atletico de Madrid.

Barcelona mabingwa watetezi wa ligi hiyo ambao watakua nyumbani kuwakaribisha klabu ya Atletico Madrid ambao wamekua kwenye ubora mkubwa siku za hivi karibuni kwenye ligi hiyo.barcelonaMchezo huo unatarajiwa kua mkali sana kwani vilabu vyote vina wachezaji wenye ubora mkubwa, Lakini kila mmoja akitafuta nafasi ya kuendelea kukaa juu ya mwenzake kwani mpaka sasa vilabu hivyo vinalingana alama.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Hispania chini ya kocha Xavi Hernandez wanakwenda kwenye mchezo huu wakiwa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya Hispania, Huku Atletico Madrid wakiwa katika nafasi ya tatu wakipishana kwa tofauti ya magoli na Barca.barcelonaMchezo wa leo unatarajiwa kua mkali na wenye ushindani mkubwa sana kutokana na mwenendo wa vilabu hivo, Barcelona wametoka kudondosha alama mchezo uliopita hivo watahitaji kupata ushindi leo vilevile Atletico Madrid wamekua kwenye fomu ya hali ya juu hivi karibuni na wanaweza kuishangaza Barca katika mchezo huu.

Acha ujumbe