Mshambuliaji wa Intermilan Lautaro Martinez amezipa kisogo tetesi zinazosema kuwa yeye atakwenda Bayern Munich ya Ujerumani au Psg ya Ufransa, huku akisema kuwa matumaini yake ni kuja kuwa Gwiji katika klabu ya Inter.

 

Martinez Anataka Kuwa Gwiji wa Inter

Chelsea, Bayern na PSG ni miongoni mwa vilabu vikubwa barani Ulaya ambavyo vimekuwa vikihusishwa mara kwa mara na mshambuliaji  huyo ambaye anatarajiwa kucheza michuano ya Kombe la Dunia akiwa na Argentina mnamo Novemba.

Huku kikosi cha Julian Nagelsmann kikisalia kuwinda mchezaji ambaye atachukua nafasi ya aliyekuwa mshambuliaji hatari wa Munich Roberto Lewandowski, huku mchezaji mwenzake Martinez wa  Argentina Lionel Messi akimvutia nyota huyo wa Inter kwenye mji mkuu wa Ufaransa.

Martinez Anataka Kuwa Gwiji wa Inter

Martinez alikanusha ripoti za kuondoka San Siro huku akielezea matarajio yake ya muda mrefu na Inter. “Sijambo, nina furaha hapa,” Martinez aliambia Rai Sport. “Natumai naweza kuwa gwiji, nina mkataba hapa na ninafikiria tu kuhusu Inter.

Martinez alifunga mabao 21 katika mechi 35 za Serie A huku Inter wakimaliza wa pili dhidi ya wapinzani wao Milan msimu uliopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alishindwa kufumania nyavu katika mechi tano mfululizo za ligi lakini alimaliza hali hiyo mbaya kwa kufunga bao dhidi ya Sassuolo Jumatano, kabla ya mabao mawili na asisti dhidi ya Fiorentina hapo jana kwenye mchezo uliomalizika kwa mabao 4-3.

Martinez Anataka Kuwa Gwiji wa Inter

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa