Klabu ya Arsenal ambayo ipo chini ya kocha mkuu Mikel Arteta wamepata sare yao ya kwanza kwenye ligi hii leo ya 1-1 kwenye mchezo wao wa raundi ya 11 dhidi ya Southampton.

 

Arsenal Yapata Sare kwa Mara ya Kwanza Msimu Huu.

Arsenal walikuwa ugenini hii leo baada ya kupata ushindi mdogo wa bao 1-0 mechi iliyopita, lakini hii leo mambo yakawa magumu dhidi ya Watakatifu wa St. Marry’s Park ambapo wameshindwa kuchukua pointi 3 muhimu.

Arsenal ndio waliotangulia kupata bao kupitia kwa mchezaji wao Granit Xhaka dakika ya 11, na baadae bao hilo lilikuja kusawazishwa na Amstrong katika dakika ya 65 ya mchezo na mpaka kipyenga cha mwisho cha mwamuzi kinapulizwa ilikuwa ni 1-1.

Lakini licha ya The Gunners kutoa sare hii leo, wameendelea kusalia kileleni wakiwa na alama 28 pointi 2 mbele ya Manchester City ambaye yupo nafasi ya pili na pointi 26 na wapo sawa michezo 11.

Arsenal Yapata Sare kwa Mara ya Kwanza Msimu Huu.

Mikel Arteta msimu huu akiwa na The Gunners ameendelea kufanya vizuri baada ya kufanya usajili muhimu katika klabu yao huku wakiwa na malengo ya kuchukua ubingwa msimu huu endapo wataweza kuendelea kufanya vizuri kuwazidi City ambao wanawafukuzia.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa