Klabu ya Arsenal imetangaza kumuongezea mkataba beki wake wa kimataifa wa Brazil Gabriel Magalhaes aambae atadumu klabuni hapo kwa muda mrefu.
Beki huyo aliejiunga na klabu ya Arsenal mwaka 2020 amekua miongoni mwa wachezaji mhimili wa klabu hiyo licha ya timu hiyo kutokua vizuri katika misimu kadhaa iliyopita lakini Gabriel alikua ni miongoni mwa wachezaji muhimu.
Mkurugenzi wa klabu hiyo ambae pia amewahi kua mchezaji ndani ya klabu hiyo amezungumza leo baada ya kutangaza kumuongezea mkataba mchezaji huyo “Ni kitu kikubwa tumekuabaliana kusaini mkataba mpya na Gabriel. bado ni mchezaji mdogo na ni sehemu ya timu yetu siku za mbeleni. Kiwango chake toka amejiunga na sisi mwaka 2020 kimekua kizuri” Alisema Edu.
Arsenal wakiongozwa na mkurugenzi wao bwana Edu wapo kwenye mchakato wa kuwaongezea mikataba mipya wachezaji wao muhimu klabuni hapo ili kutengeneza timu imara siku mbeleni kwenye timu hiyo.

