Anchelotti: Naamini Toni Atasaini Mkataba Mpya.

Kocha wa Real Madrid Carlo Anchelotti amesema anaamini kiungo wa klabu hiyo Toni Kroos raia wa Ujerumani atasaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo na kuendelea kuitumikia Real Madrid.

Toni Kroos mkataba wake unamalizika mwezi Juni mwaka 2023 yaani mwisho wa msimu huu hivo kama atasaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo utamfanya kuendelea kusalia klabuni hapo jambo ambalo kocha Anchelotti anaamini kiungo huyo atalifanya.anchelottiKroos ambae alishawhi kubainisha anataka kustaafia klabuni hapo pale atakapomaliza kucheza mpira huku akiwa tayari ameshataafu timu ya taifa ya Ujerumani na ikitokea ameshindwa kuongeza mkataba basi atastaafia pia klabuni hapo mwisho mwa msimu wa 2022/23.

“Atafikiaria hilo Januari,Febuari. yeye mwenyewe. Nafikiri Toni ataendelea kubakia ndani ya Real Madrid. Ni maamuzi yake, Tutaona itakuaje. Atafikiria kuhusiana na hilo halafu atatangaza kaamua nini” Alsema Anchelotti akizungumzia suala Toni kuongeza mkataba.anchelottiToni Kroos ni miongoni mwa wachezaji waliodumu kwea muda sasa ndani ya klabu ya Real Madrid ni kupata mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.