Mason Greenwood Arejeshwa kwenye Kikosi United

Klabu ya Manchester United imemrejesha mshambuliaji wake wa kimataifa wa Uingereza Mason Greenwood kwenye kikosi ambacho kitatumika msimu ujao kwenye michuano mbalimbali.

Mason Greenwood ameonekana leo kwenye tovuti ya klabu ya Man United akiwa miongoni mwa wachezaji waliobakizwa kwajili ya msimu ujao, Huku wachezaji wengine wakiruhusiwa kuondoka ndani ya klabu hiyo jambo ambalo limeibua hisia kwa mashabiki wa klabu hiyo.Mason GreenwoodKinda huyo ambaye amekua nje ya uwanja kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kijinsia ambao ulikua unamkabili, Lakini alifanikiwa kuachiwa huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi kwa upande wa washitaki.

Kurejea kwa Mason Greenwood kwenye kikosi cha Manchester United ni furaha kubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo, Kwani mchezaji huyo ana kipaji kikubwa na alikua anatazamiwa kufanya makubwa siku za usoni kabla ya kukutwa na tuhuma hizo.Mason GreenwoodKocha wa Manchester United Erik Ten Hag alishabainisha kua anamuhitaji Mason Greenwood kwakua ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa, Lakini akisisitiza maamuzi hayapo mikononi kwake hivo atahitaji kusubiri maamuzi kutoka ngazi ya juu kujua mchezaji huyo atabaki au ataondolewa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.