Saliba Mambo Shawari Arsenal

Beki wa klabu ya Arsenal raia wa kimataifa wa Ufaransa William Saliba anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuwatumikia washika mitutu hao kutoka jiji la London kwa muda mrefu zaidi.

Mkataba wa Saliba na klabu ya Arsenal ulikua unamalizika mwaka 2024 lakini beki huyo ameongeza mkataba wa muda mrefu kuendelea kubaki kwenye viunga vya Emirates mpaka mwaka 2027 na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja mpaka 2028.SalibaBeki huyo wa kimataifa wa Ufaransa amekua kwenye kiwango kikubwa tangu arudi ndani ya klabu hiyo akitokea nchini Ufaransa ambapo alikua kwa mkopo, Kitu ambacho kiliwavutia Arsenal kumuongezea mkataba wa muda mrefu.

Beki Saliba atasaini mkataba huo akirudi kutoka mapumzikoni kwani mpaka sasa makubaliano ya kila pande tayari yameshafikiwa kinachosubiriwa ni beki huyo kumwaga wino ambapo atakuwepo klabuni hapo mpaka 2027.SalibaArsenal wanahitaji kuiboresha timu hiyo na kurudi kua timu yenye ushindani mkubwa kuanzia Uingereza na ulaya nzima chini ya kocha Mikel Arteta, Huku moja ya mipango ni kuwapa mikataba wachezaji wao muhimu Saliba akiwa miongoni mwao.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.