Kaka yake Paul Pogba,  Mathias Pogba amefunguliwa mashitaka kwa tuhuma za utapeli kwa kaka yake Paul Pogba ambaye ni kiungo wa Taifa la Ufaransa na klabu ya Juventus ambapo alijiunga nayo msimu huu.

 

Mathias Pogba Akusudia Kukataa Rufaa

Uchunguzi huo ulifunguliwa mwezi uliopita kuhusu madai ya Paul kwamba likuwa mlengwa wa njama ya unyang’anyi wa kaka yake na marafiki zake wa utotoni wakidai kiasi cha Euro milioni 13. Mathias ambaye ni mchezaji huru baada ya kucheza na timu ya daraja la nne ya Ufaransa Belfort kumalizika mwezi April alitishia kusambaza “Ufichuzi wa kusambaa” video iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 32 amekana kushiriki katika majaribio ya unyang’anyi dhidi ya kaka yake ambapo Jumamosi taarifa ziliibuka kuwa  yeye na wenzake wanne wamefunguliwa mashitaka na sasa na watakuwa wakishikiliwa jela huku wakisubiri uamuzi kutoka kwa hakimu kuhusu kutoka kwa dhamana.

 

Mathias Pogba Akusudia Kukataa Rufaa

 

Wakili wa Mathias alithibitisha kwenye kituoa cha Ufaransa cha BFMTV kwamba mteja wake anakusudia kupinga uamuzi huo alisema kuwa;

“Ni uamuzi ambao hatuelewi hasa kwasababu mahakama imetambua Bwana Mathias hakushiriki katika vitendo vya utekaji nyara, ambavyo kaka yake alidaiwa kuwa ni mhanga wa tukio hilo”. Wakili huo alisema.

Bwana  Pogba angeweza kabisa na alipaswa kuachiliwa wakati wa uchunguzi huu wa mahakama. Kwahiyo hilo halitaishia hapo, tutapinga uamuzi huu kwa mtazamo wa kisheria ili Bwana Mathias Pogba aachiliwe haraka iwezekanavyo.

Wakili alikazana kwa kusema kuwa Mathias ni mtu safi, ana rekodi safi ya uhalifu, sio jambazi  hana hatia na pia kwa mtu ambaye hakutenda kosa kuishia gerezani ni jambo gumu sana, kwahiyo tutapambana ili atoke haraka iwezekanavyo.

 

Mathias Pogba Akusudia Kukataa Rufaa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa