Mechezaji wa Stoke City James McClean, amelimwa faini kutokana na kuchapisha chapisho linalodaiwa kuwa na maudhi na kuamsha hisia tofauti. Nyota huyu alilimwa faini na Klabu yake ya mshahara wake wa wiki mbili na amekubali kufuta akaunti yake ya Instagram baada ya kuchapisha picha na maneno yaliyochukuliwa kuudhi.
Wakati kukiwa na jitihada za kupambana na janga la virusi vya corona, moja ya hatua zinazosisitizwa zaidi ni kujiweka umbali kiasi na watu wengine kuepusha uwezekano wa maambukizi ya virusi hivyo. Nyota huyu alichapisha picha kwenye sehemu ya stori ya akaunti yake iliyoibua utata.
Munekano wa picha aliyochapisha alikuwa ni yeye mwenyewe akiwa mbele ya watoto wawili wasichana na akiwa amevalia maski nyeusi inayoziba sehemu ya uso na kuacha macho na mdomo (kama ninja). Kisha aliandika maneno yanayosomeka kwa kiingereza kuwa “Todays School lesson -History” akimaanisha “Somo la leo Shuleni -Historia”.

Chapisho lake linatajwa kuibua sintofahamu na hisia za watu na kuhusishwa kwake kuwa alikuwa anakejeli jeshi la IRA kwa maski za kujiziba uso, kama alivyoonekana yeye kwenye picha. Hii imeonekana kuwa nyota huyu alikuwa na nia ovu na chapisho lake lililenga kukejeli na kuudhi. Hii ndiyo sababu klabu yake imeamua kumchukulia hatua ya kumlipisha faini.
McClean amekiri na kuomba radhi, lakini amesisitiza kuwa awali hakudhani kama chapisho
hilo lingechukuliwa kuwa linaudhi au kejeli. Hata hivyo amebainisha kuwa amefanya mazungumzo na klabu na anatarajia kufuta akaunti yake ya Instagram.

