Mctominay,Lindelof Hatma Yao Kujulikana Mwisho wa Msimu

Wachezaji wawili wa klabu ya Manchester United Scott Mctominay na beki Victor Lindelof hatma yao kuamuliwa mwishoni mwa msimu huu na kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag ambaye ataamua kama ataendelea kuwatumia wachezaji hao.

Scott Mctominay amekua hapati nafasi ya kuanza mara kwa mara ndani ya msimu huu baada ujio wa viungo kama Casemiro na Christian Eriksen kufika ndani ya timu hiyo, Hivo kufanya kiungo huyo kufikria kuondoka ndani ya miamba hiyo ya ligi kuu Uingereza.MctominayBeki wa klabu ya Manchester United Victor Lindelof nae amekua hayupo kwenye matumizi ya mara kwa mara kwa kocha Erik Ten Hag ambaye amekua akiwatumia Lisandro Martinez, na Raphael Varane mara kwa mara jambo linaweza kumfanya beki huyo kutimka ndani ya majira ya joto.

Scott Mctominay amekua akivivutia vilabu kadhaa ndani ya ligi kuu ya Uingereza na mojawapo ni klabu ya Newcastle United, Kocha wa klabu ya Newcastle Eddie Howe inaelezwa anamfatilia kiungo huyo kwa ukaribu zaidi hivo kama itatokea ataondoka ndani ya United basi Newcastle United ndio mahala anaweza kutimkia.MctominayKocha Erik Ten Hag ndio ataamua Mctominay na Lindelof kama watandelea kubaki ndani ya klabu ya Manchester United mwishoni mwa msimu kwani kama kocha huyo ataona kua wachezaji hao wanastahili kuendelea kuitumikia klabu hiyo basi wataendelea kuwepo, Lakini kama ataona ni muda wa kuondoka kwa wachezaji hao basi milango itakua wazi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.