Luca Modric na David Alaba watakwenda kumenyana katika mchezo wa Uefa Nations League utakaozikutanisha timu zao za Croatia na Austria usiku wa leo.

Wachezaji hao wanaocheza pamoja katika ngazi ya klabu wakiwa wanawatumikia mabingwa wa ulaya klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania lakini leo kila mmoja atakua akihahakisha analipambania taifa lake liweze kupata matokeo katika mchezo huo.

modricMchezo wa kwanza uliopigwa mwezi juni mwaka huu uliozikutanisha timu hizo uliisha kwa Austria kushinda kwa mabao matatu kwa bila huku Croatia wakiwa nyumbani mchezo wa leo unatazamiwa kua na mvuto kwani Austria wanatafuta ushindi ili waweze kutoka mkiani mwa kundi hilo huku Croatia nao wahihitaji kufuta uteja baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Austria.

 

Austria wakiwa wanashika mkiani katika kundi namba moja wanahitaji alama tatu muhimu usiku wa leo wakiwa nyumbani ili kutoka mkiani walipo sasa,Vijana hao wa Ralf Rangnick wameshinda mchezo mmoja kati ya mitano waliocheza,wamesuluhu mmoja na kupoteza mitatu hivo mchezo wa leo unaweza kua nafasi ya wao kubadili upepo mbaya waliokua nao.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa