Eliud Kipchoge mwanariadha maarufu wa mbio ndefu kutoka nchini Kenya amefanikiwa kuvunja rekodi yake mwenyewe aliowahi kuiweka miaka minne nyuma.

Bingwa huyo mara mbili wa michuano ya olimpiki amevunja rekodi hiyo mchana wa leo katika mbio zilizofanyika katika jiji la Berlin mchana wa leo.

Raia huyo wa Kenya alishinda mbio hizo kwa kutumia masaa mawili,dakika moja na sekunde tisa na kuishinda rekodi yake ya awali kwa sekundi thelathini na kuendelea kutengeneza rekodi kila siku kutoka na ubora anaounesha katika mchezo huo.

eliud kipchogeKipchoge baada ya kushinda mbio hizo ameweza kuzungumza “Nimefurahishwa na maandalizi yangu na nafikiri nilikua na kasi kwasababu ya ushirikiano wa pamoja na timu yangu,Kwasababu kila kitu kinategemea ushirikiano”

“Kinachonipa motisha ni familia yangu, na nataka kuwapa moyo vijana kwasababu mchezo unaunganisha watu na hilo pia ndo linalonipa motisha”

Kushinda marathoni hii kunamfanya Kipchoge kushinda marathoni 15 kati ya 17 alizowahi kushiriki katika maisha na inaonesha ni kwa kiwango gani mwanaridha huyo ana ubora.

Eliud Kipchoge anaendelea kuupa uhai msemo unaosema mtu pekee unaepaswa kushindana nae basi ni wewe mwenyewe.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa