Ali Kamwe mwandishi na mchambuzi wa soka katika kituo cha Azam Media inasemekana anakaribia kutangazwa kama Afisa Habari mpya katika klabu ya Yanga.

Baada ya aliekua afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli klabuni hapo klabu hiyo ilitangaza nafasi ya kazi katika eneo hilo na watu mbalimbali wenye sifa kutuma maombi ili kupata nafasi hiyo na miongoni mwa waliotuma maombi hayo inaelezwa Ali Kamwe ni miongoni mwao.

ali kamweMchambuzi huyo aliejizolea umaarufu mkubwa zaidi katika kuchambua soka la nyumbani pamoja na kwenye mitandao yake kijamii baada ya kuja na uchambuzi wake baada ya mechi uliojulikana kama mambo 10 ya Ali Kamwe.

Mpaka sasa inasemekana miongoni mwa waliotuma maombi ya nafasi hiyo jina la mchambuzi huyo lipo kileleni kabisa na kama mambo yatabaki hivihivi basi siku yoyote mwandishi huyo atatangazwa rasmi kama mrithi wa Hassan Bumbuli katika timu hiyo ya wananchi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa