WAKATI wakijiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal ya Sudan, Benchi la ufundi la Yanga limefunguka kuwa mchezo huo utakuwa mgumu hivyo wamejipanga kwa ajili ya kuhakikisha wanapata nafasi ya kuingia hatua ya makundi.

Yanga wamepata nafasi ya kusonga katika raundi ya kwanza baada ya kuifunga Zalan kwa jumla ya mabao 9:0.

Yanga, Yanga Yaihofia Al Hilal, Meridianbet

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa: “Mchezo uliopita dhidi ya Zalan ulikuwa mgumu katika kipindi cha kwanza kwani tulikuwa hatuwajui vyema wapinzani wetu.

“Kwa sasa maandalizi yanaendelea kuelekea mchezo wa raundi ya kwanza dhidi ya Al Hilal, tunajua mchezo utakuwa mgumu kwenye Uwanja wa hapa nyumbani na ule wa ugenini.

“Mipango yetu ya kwanza ni kuingia katika hatua ya makundi na tunahitaji kupata matokeo katika mchezo huu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa