WACHEZAJI wa KMC leo wameanza maandalizi kuelekea katika mchezo unaofuata wa Ligi Kuu dhidi ya Namungo ambao utapigwa Oktoba 1, mwaka huu kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini kwa upande wao wataenda kupambana kwa ajili ya kuhakikisha wanapata pointi tatu.

“Tulipokea taarifa ya mabadiliko ya mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao awali ilikuwa tucheze siku ya Jumanne ya Septemba 27 kwenye uwanja wetu wa Uhuru, kwa hiyo hivi sasa tunajiandaa kwa mchezo mwingine ambao tutakuwa ugenini dhidi ya Namungo hivyo tunajipanga kutafuta pointi tatu muhimu ugenini.

“Wachezaji wote wamerejea kambini baada ya kumaliza mapumziko ya siku mbili ambayo tulitoa siku tuliyocheza mechi na Ihefu, na wote wamerejea salama wakiwa na nguvu, Afya njema, ari na morali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunafanya maandalizi bora ambayo yatatupa matokeo chanya kwenye mchezo huo licha ya kwamba tunafahamu fika hautakuwa mepesi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa