Mohamed Salah Mchezaji Bora Novemba

Staa wa klabu ya Liverpool raia wa kimataifa wa Misri Mohamed Salah amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa ligi kuu ya Uingereza kwa mwezi Novemba kutokana na kiwango bora alichokionesha ndani ya mwezi huo.

Mohamed Salah amekua kwenye kiwango bora sana msimu huu akiwa ameshafanikiwa kufunga mabao 13 na kutoa pasi nane za mabao jambo ambalo linamfanya aendelee kua mchezaji muhimu zaidi kwenye kikosi cha Liverpool chini ya kocha Arne Slot ambacho ndio vinara wa ligi kuu ya Uingereza mpaka sasa.mohamed salahKwenye mwezi husika yaani mwezi Novemba mshambuliaji huyo amehusika kwenye mabao matano ambapo alifanikiwa kufunga mabao manne kwenye na kupiga pasi moja ya bao, Katika michezo yote mitatu iliyochezwa ndani ya mwezi Novemba mchezaji huyo alifanikiwa kufunga katika michezo yote na kupiga pasi ya bao katika mchezo mmoja.

Kutokana na takwimu ambazo Mohamed Salah amekua nazo ndani ya mwezi Novemba ni wazi amestahili kunyakua tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi Novemba ndani ya ligi kuu ya Uingereza akiwashinda wachezaji wenzake ambao alikua anawania nao tuzo hiyo kama Bukayo Saka, Martin Odegaard, Matheus Cunha, Ryan Gravenberch, Yvone Wissa, pamoja na Joao Pedro.

 

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.