Mourinho Afichua Kuwa Spurs ni Klabu Pekee Ambayo Hana Hisia Nayo Sasa

Jose Mourinho amedai Tottenham ndio klabu yake pekee ya zamani ambayo hana uhusiano wowote nayo.

 

Mourinho Afichua Kuwa Spurs ni Klabu Pekee Ambayo Hana Hisia Nayo Sasa

Mreno huyo mwenye miaka 60, alikaa kwa miezi 17 Spurs lakini alitimuliwa na mwenyekiti Daniel Levy mnamo Aprili 2021 wiki moja tu kabla ya kucheza na Manchester City kwenye fainali ya Kombe la Carabao.

Mourinho aliwahi kuwa kocha wa Porto, Chelsea, Inter Milan, Real Madrid na Manchester United.

Baadaye alichukua usukani wa klabu ya Roma, na kushinda Ligi ya Europa Conference na kuwaongoza hadi fainali ya Ligi ya Europa msimu huu, ambapo watacheza na Sevilla Jumatano ijayo.

Mourinho Afichua Kuwa Spurs ni Klabu Pekee Ambayo Hana Hisia Nayo Sasa

Akiongea kabla ya mechi hiyo, Mourinho alisema: “Natumai mashabiki wa Tottenham hawatanielewa vibaya lakini klabu pekee katika maisha yangu ya soka ambayo bado sina hisia za ndani ni Tottenham. Labda kwa sababu uwanja ulikuwa tupu, wakati wa Covid. Labda kwa sababu Bw Levy hakuniruhusu kushinda fainali na kushinda kombe.”

Mourinho, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Paris Saint-Germain msimu huu wa joto, alikuwa akijibu swali kuhusu mustakabali wake na Roma.

Aliongeza: Tutaunganishwa milele, kama nilivyo na vilabu vyangu vyote vya awali, mbali na klabu ya Mr Levy.

Mourinho Afichua Kuwa Spurs ni Klabu Pekee Ambayo Hana Hisia Nayo Sasa

“Ni pekee, kwa hivyo baada ya hapo Porto, Chelsea, Inter, Real Madrid, Manchester United vilabu vyote ninahisi uhusiano. Labda watu watasema huwezi kupenda kila klabu ndiyo, napenda kila klabu.” Alisema Mourinho.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.