Klabu ya Mtibwa Sugar imesema kwamba, ipo kwenye hatua nzuri ya kuufanyia marekebisho uwanja wao wa Manungu ili waweze kuutumia kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara.
Uwanja huo wa nyumbani wa Mtibwa, ulifungiwa msimu uliopita na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutokana na kutokidhi vigezo na kuifanya timu hiyo kubadilisha uwanja kwa kuutumia Uwanja wa Jamhuri.
Msimu huu, Mtibwa Sugar imeshindwa pia kuutumia Uwanja wa Jamhuri, ambapo katika mechi zake mbili za kwanza za Ligi Kuu Bara, imetumia Uwanja wa Mabatini uliopo Pwani na Uhuru, Dar.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema: “Kuhusu uwanja wetu wa Manungu uliopo Turiani, tumeshakamilisha marekebisho ya eneo la kuchezea na tayari tumeweka uzio.
“Kinachoendelea kwa sasa ni ujenzi wa ukuta ambao utachukua wiki nne kukamilika, hivyo tunatarajia mechi za Simba SC na Yanga SC tutacheza kwenye uwanja wetu.”
SPACE SPIN NA MERIDIANBET.
Ni Mabingwa pekee Meridianbet wanakupa nafasi ya kushinda zaidi na mchezo wa Space Spin katika kasino bomba za meridianbet. Ni wakati wa kufurahia na kutengeza mkwanja bila kuwaza.