Newcastle: The Big Fish In The Transfer Market.

Mpaka sasa, hakuna klabu inayofanya vizuri sokoni kuizidi Newcastle United. Japokuwa wanahali mbaya kwenye msimamo wa EPL lakini, wanamvuto sokoni. 

Mpaka sasa, Newcastle United wameshasajili wachezaji watatu – Kieran Trippier, Chris Woods na Bruno Guimaraes. Lakini, kuna uwezekano wakasajili wachezaji zaidi kuelekea mwishoni mwa dirisha la usajili.

Baadhi ya sajili zipo mbioni kukamilika – Dan Burn, Matt Targett na Hugo Ekitike. Pamoja na hawa, Jesse Lingard bado anahusishwa na The Magpies. Je, ni suala la muda au mambo yatakuaje?

Hugo Ekitike

Inasemekana, kuna vitu viwili vinahusika kwenye usajili wa Ekitike na Lingard. Moja, japokuwa kuna makubaliano ya vilabu (United na Reims), Ekitike hajashawishika kwenda St. James’ Park na hivyo, itahitajika nguvu ya ziada kumvuta.

Wakati muda ukiwa unazidi kwenda, na uhalisia kuwa Ekitike yupo Ufaransa. Huenda ikawa ni changamoto kukamilisha usajili huu ndani ya saa chache zilizobaki.

Jesse Lingard.

Kitu cha pili ni matakwa ya kifedha kwenye usajili wa Lingard. Man United wanataka walipwe ada ya usajili wa mkopo pamoja na uwepo wa kipengele cha kulipwa £12M, endapo The Magpies watafanikiwa kubaki kwenye EPL msimu huu.

Lingard kwa upande wake yupo tayari kwenda Newcastle United na sasa, kazi ipo kwa Eddie Howe na viongozi wake kufanikisha hilo.


 

VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.