Golikipa mpya wa klabu ya Manchester United Andre Onana ameanza na kipigo ndani ya klabu hiyo baada ya jana klabu yake kupokea kipigo mbele ya Real Madrid.
Onana wakati anacheza mchezo wake wa kwanza na Man United uliopigwa usiku wa kuamkia leo nchini Marekani alijikuta anaruhusu nyavu zake kuguswa mara mbili ambapo Real Madrid walishinda kwa mabao mawili kwa bila katika mchezo huo.Mabao ya Real Madrid katika mchezo wa jana yote yalifungwa na wachezaji wapya ndani ya klabu hiyo ambao ni Jude Bellingham aliefunga bao la kwanza pamoja na mshambuliaji Joselu na kuipa ushindi klabu hiyo dhidi ya Man United.
Licha ya kuruhusu mabao mawili katika mchezo wa jana Onana amejizolea sifa kedekede katika mchezo kama kawaida yake ameonesha uwezo mkubwa katika kupiga pasi sahihi na kuanzisha mashambulizi kuanzia nyuma.Wachezaji wenzake pia kwenye kikosi hicho wamemsifu kutokana na uwezo wake wa kucheza kuanzia nyuma akiwemo beki wa kushoto wa klabu hiyo ambaye amesema kipa huyo amewafanya kama mabeki kujiamni kutokana na uwezo wake na utulivu mkubwa alionao.