Palmer Azidi Kuitesa Man United, Thamani Yake Yafika Pauni Milioni 150

Klabu ya Manchester United huenda ikalazimika kuvunja rekodi ya uhamisho wa mchezaji wa Uingereza Cole Palmer kwa dau la zaidi ya pauni milioni 150 iwapo itataka kumnasa kiungo huyo mshambuliaji wa Chelsea.

Palmer, mzaliwa wa Wythenshawe, amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea Kaskazini Magharibi mwa England alijiunga na Chelsea mwaka 2023 akitokea Manchester City kwa dau la pauni milioni 40. Akiwa Etihad, alishinda mataji ya Premier League na UEFA Champions League, lakini alipata nafasi ndogo ya kucheza, akiishia mechi 41 pekee za kikosi cha wakubwa.

Palmer Azidi Kuitesa Man United, Thamani Yake Yafika Pauni Milioni 150

Katika msimu wake wa kwanza Stamford Bridge, alifunga mabao 25 na kutwaa tuzo ya PFA Young Player of the Year. Tangu hapo ameongeza mataji ya UEFA Europa Conference League na FIFA Club World Cup, jambo linaloifanya Chelsea kuona thamani kubwa katika uwekezaji wao.

Hata hivyo kw sasa, Palmer ana mkataba wakuitumikia Chelsea hadi mwaka 2033, hali inayomaanisha klabu hiyo inaweza kudai zaidi ya mara tatu ya dau walilomnunua kwa Timu yoyote itakayohitaji huduma yake.

Palmer Azidi Kuitesa Man United, Thamani Yake Yafika Pauni Milioni 150

Ripoti zimekuwa zikidai kuwa kiungo huyo amekuwa akijihisi kutamani kurejea nyumbani, lakini mwenyewe alikanusha uvumi huo kwa kusema; “Watu wanapenda kuzungumza mambo yasiyo ya kweli. Mimi sipewi sana uzito na maneno hayo.” Amesema palmer

Na Kwa upande wake mchezaji wa zamani wa Chelsea Frank Sinclair pia alipuuza tetesi hizo, akieleza kuwa hana wasiwasi iwapo Palmer ataondoka na amesema dili hilo ni gumu kutokea kwa sasa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Sina wasiwasi na uvumi, isipokuwa kama unatoka kwake mwenyewe. Nadhani ana furaha klabuni na sioni dalili za yeye kuondoka,” alisema Sinclair.

Palmer Azidi Kuitesa Man United, Thamani Yake Yafika Pauni Milioni 150

Aliongeza kuwa London ni miongoni mwa miji bora kwa mchezaji kuishi na kwamba changamoto kubwa kwa kiungo huyo msimu huu imekuwa ni majeraha na kukosa mwendelezo wa mechi, jambo lililoathiri kiwango chake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.