Wakati ligi nyingi zikiendelea kutangaza mabingwa wa ligi hizo, mambo hayakuwa hivyo kwenye EPL, ambapo penati ya Paneka aliyopiga Kun Aguero iliwagharimu Manchester City na kuwafanya wapoteze mchezo huo kwa goli 2-1.

Chelsea walikuwa wageni wa Manchester City katika mechi ya EPL hapo jana, mchezo uliojawa na mashambulizi yakupokezana kwa timu zote mbili huku City wakiongeza kupiga idadi ya mashuti 16 dhidi ya 12 ya Chelsea.

Safu ya ushambuliaji ya City chini ya Aguero ilionekana kuwa butu huku wakipiga mashuti 4 tu yaliyolenga lango, huku Chelsea wao wakipiga 5. Aguero aligeuka mada ya mchezo baada ya kupiga penati kwa mtindo wa Paneka ambayo iligeuka kuwa ‘chakula’ kwa Mendy.

Gabriel Jesus wa City alichezewa rafu na Alonso katika eneo la 18, na kusababisha peneti hiyo ambayo imeonekana kupingwa na kusemwa na watu wengi sana duniani. City walihitaji kushinda mechi hiyo tu ili waweze kutangazwa mabingwa lakini badala yake wakawapa Chelsea moyo kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa baadae wiki hii.

Wachezaji wenzake walisema Aguero hajawahi kufunga paneka hata kwenye mazoezi, hivyo ule ulikuwa ni uamuzi wa kijinga sana hasa kwa timu inapojaribu kukusanya alama nyingi kadri iwezavyo.

Kocha wa City, Pep Guardiola alimkingia kifua na kusema kwamba linapokuja suala la kupiga penati huwa anawaruhusu wachezaji wake wapige namna watakavyolakini wadhamirie, na kama Aguero alidhamiria kufunga basi kama amekosa ni sehemu ya mchezo tu!

Baada ya mechi, Aguero alitoa ujumbe wa kuomba radhi kwa wachezaji wenzake na mashabiki kwa kukosa penati ambayo ilikuwa muhimu sana kurudisha timu kwenye moto wa kusaka ubingwa, kwa kuchagua paneka hali ya kuwa hakuwahi piga.

Chelsea na Manchester City watakutana tena katika fainali ya Champions league tarehe 29 mwezi huu. Bado haijajulikana ni uwanja gani utatumika kutokana na ule wa awali kule Instabul kutiliwa shaka baada ya Uturuki kuwekewa vikwazo na Uingereza.


TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO

Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!

paneka, Paneka ya Aguero Yaigharimu City, Meridianbet

SOMA ZAIDI

15 MAONI

  1. Safu ya ushambuliaji ya City chini ya Aguero ilionekana kuwa butu huku wakipiga mashuti 4 tu yaliyolenga lango, huku Chelsea wao wakipiga 5. Aguero aligeuka mada ya mchezo baada ya kupiga penati kwa mtindo wa Paneka ambayo iligeuka kuwa ‘chakula’ kwa Mendy.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa