Paul Merson amiambia klabu ya Arsenal kutompa mkataba mpya mshambuliaji wao Alexandre Lacazette na kumuacha aondoke mwishoni mwa msimu japokuwa yupo kwenye kiwango kizuri hivi karibuni.

Mkataba wa mshambuliaji huyo unamalizika mwisho wa msimu huu majira ya kiangazi na kwa sasa yupo huru kufanya makubaliano na klabu yeyote ile ikiwa atahitaji kufanya hivyo.

Paul Merson
Paul Merson

Paul Merson ameionya klabu yake hiyo ya zamani ili yasitokee kama yaliotokea kwa mshambuliaji mwenza Aubameyang huku akinukuliwa akisema, “kama Lacazette akiendelea na kiwango hichi na akafanikiwa kufungu goli 10 kabla ya msimu kuisha, Arsenal watapata uchizi na kumpa mkataba mpya wenye thamani ya  £250,000 kwa wiki.

“Arsenal wanachopaswa kufanya ni kuzuia, kisije kutokea kama kilichotokea miaka mingi iliyopita, ambapo Arsenal walikuwa na vijana bora sana uwanjani lakini ghafla unasikia kuna mkutano na tayari wameshaondoka.

“Hilo halipaswi kutokea, Arsenal inabidi waboreshe mikataba ya wachezaji wenye umri mdogo  na wanawachezaji wazuri tu vijana, Arsenal hawawezi kukabwete tu kwa wachezaji ambao muda wao unafika mwishoni na kuwaacha vijana wanaondoka bure.”


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa