Tumaini Jipya kwa Philipe Countinho Barcelona 2021/22

Philipe Countinho yupo katika nafasi ya kupata wakati mwingi zaidi wa kucheza na kurejesha umuhimu wake msimu huu.

Nyota huyu wa Brazil amekuwa na kipindi kigumu tangia alipowasili klabuni hapo kwa uhamisho wa pesa nyingi Camp Nou mwaka 2018 akitokea Liverpool.

Alitumia mwaka mmoja kwa mkopo kule Bayern Munich, akifanikiwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa, na kujikuta kwenye mkwamo wa majeraha na kuwa kwenye fomu nzuri.

Tumaini Jipya kwa Philipe Countinho Barcelona
Philipe Countinho

Countinho sasa amerejea akiwa fiti, na tayari ameshaanza kucheza mechi na kikosi chake cha Barcelona akitokea benchi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa, ambayo walipoteza dhidi ya Bayern.

Kwa mujibu wa chapisho la Marca, Countinho sasa anatarajiwa kucheza gemu nyingi zaidi chini ya Ronald Koeman, kikosi ambacho kwa siku za hivi karibuni kimeonekana kupungua ubora.

Philipe Countinho  anamaliza mkataba wake wa sasa na Barcelona mwaka 2023, na msimu ujao utakuwa msimu muhimu zaidi katika maisha yake ya soka ili kujua kesho yake.

Barcelona wanaweza kufanya maamuzi msimu ujao wa joto, ikiwa wasalie na nyota huyu au wamuweke sokoni.


MKWANJA NJE NJE NA DISCO FUNK

Unaanzaje siku yako na kuimaliza bila kupitia katika kasino bomba za meridianbettz, mchezo mashuhuri wa Disco Funk unaweza kukufanya uwe mshindi leo hii!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.