Pogba: "Sijaridhika Kabisa, Nahitaji Mataji"

Iwe ni Manchester United, au nje ya Manchester United, Paul Pogba anataka kushinda mataji. Hili ni suala la ambalo kila mchezaji makini analitaka.

Mchezaji huyu wa Ufaransa, anasema kuwa hajaridhika na kipindi chote cha misimu mitano aliyokuwepo Manchester United, wakati timu hii ikiwa na ukame wa mataji.

Pogba: "Sijaridhika Kabisa, Nahitaji Mataji"

Inakumbukwa staa huyu alisajiliwa kwa £89m, baada ya kuwa na misimu minne ya mafanikio ya mataji kule Juventus. EFL Cup na Europa League ndiyo mataji pekee aliyonayo Pogba akiwa na Manchester United.

Staa huyu mwenye umri wa miaka 29, anatarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu pale mkataba wake unapomalizika huku Juventus na Barcelona wakitajwa kuihitaji huduma yake.

Staa huyu alieleza kwa uchungu juu ya wakati wake aliokuwa United, kwa kuanzia msimu huu;

“Inabidi kuwa wakweli. Sijaridhika kwa kipindi chote cha miaka mitano iliyopita, hata kidogo. Mwaka huu pia umepotea. hakuna taji tunaloshinda kwa mara nyingine tena. Iwe ni Manchester United, au kwingine ninataka kushinda mataji.” – Paul Pogba


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe