Chama cha soka nchini Uingereza FA na vyama vya soka vya Ireland ya kaskazini, jamhuri ya Ireland, Scotland na Wales leo wamewasilisha pendekezo la kuandaa mashindano ya UEFA Euro 2028 kwa pamoja kwenye shirikisho la mpira wa miguu barani Ulaya.
Muungano wa mashirikisho hayo matano walitoa waraka ambao ulisomeka, “Tunaamini Euro 2028 itakuwa moja tukio la kimichezo bora ambalo halikuwai kuandaliwa na Uingereza na Ireland.
“Muungano huu wa mashirikisho matamo ni bora usio na kifani ambao umeandaa kitu maalum kwa ajiri ya mpira wa miguu, ikiwemo uhakika wa upanuzi wa mashindano, na tunahusudu kufikia matarajio na kuacha alama kwa watu wote wa Uingereza na Ireland.”
Uingereza na Ireland waliachana na mpango wa kutaka kuandaa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2030, mwezi uliopita kwa ajiri ya kutaka kuandaa mashindano ya Euro 2028.
UEFA imepanga kutanaua wigo wa mashindano hayo kwa kuongeza idadi ya timu na kufika timu 32, huku majibu kamili yanatarajiwa kutoka 7 April baada ya kukubaliana na wanachama wa shirikisho hilo.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.