Poland itakataa kucheza mechi zijazo za mchujo za Kombe la Dunia dhidi ya Urusi mwezi Machi kufuatia nchi hiyo kuivamia Ukraine.

 

poland, Poland Kugomea Mechi dhidi ya Urusi., Meridianbet

Washindi wa mchezo huo ambao ulipaswa kuchezwa Machi 25, wangemenyana na Sweden au Jamhuri ya Czech siku nne baadaye kuwania kufuzu kwa fainali itakayofanyika Qatar mwezi Novemba.

Chama cha Soka (FA) cha Poland pia kimejitolea kuandaa mechi zote za nyumbani za Ukraine huku Ukraine ikishindwa kucheza katika nchi yao.

Ukraine wanatazamiwa kucheza na Scotland katika mchujo wa kuwania kombe la dunia huko Hampden Park mnamo Machi 24, na mshindi atacheza na Wales au Austria mjini Cardiff au Vienna mnamo Machi 28.

Msemaji wa FA wa Poland ameiambia Sky Sports News: “Hakuna maneno zaidi, ni wakati wa kuchukua hatua. Kutokana na kukithiri kwa uchokozi wa Shirikisho la Urusi dhidi ya Ukraine, timu ya taifa ya Poland haina nia ya kucheza mechi ya mtoano dhidi ya Urusi.

“Huu ndio uamuzi pekee sahihi. Tunafanya mazungumzo na mashirikisho ya Sweden na Czech ili kuleta msimamo wa pamoja kwa FIFA.” aliongeza taarifa hiyo.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa