Kuna taarifa imefichuka kuwa Ligi Kuu ya Uingereza inafikiria kuonesha gemu bure pale msimu utakaporejea tena hewani.
Kwa sasa BT Sport na Sky Sports wanalipa kiasi kikubwa cha pesa kupata haki ya kuonesha gemu hizo za ligi kubwa huko Uingereza lakini pia Premier League wanaweza kuja na mfumo mwingine wakati ligi zitakaporejea tena viwanjani.
Kwa mujibu wa katibu wa mambo ya utamaduni wao, Oliver Dowden, ni kuwa Premier League wanaangalia namna ya kutangaza gemu hizo zilizosalia bure kabisa kwenye televisheni mbalimbali.
Akiongea kwenye mkutano wa wanautamaduni, habari na michezo siku ya Jumatatu, Dowden alisema: “NI kitu kizuri saba na nimetoa rai yangu kwa Premier League katika mazungumzo yetu juu ya hili.
“Nimewaambia Premier League kwa kinagaubaga kuwa ninafikiri kwamba itakuwa inaleta ujumbe maalum kwamba wao ni kama wa kwanza kurudi hewani wakicheza bila ya mashabiki uwanjani na watu wengi hawatoweza kuwaona na kupata huduma hiyo.
“Ninatambua kwamba michezo inategemea mapato ya matangazo kujiendesha na sitotaka kufanya tofauti na hivyo katika mamlaka yangu nikijaribu kubadili vitu hivyo.
“Lakini wanatambua fika kwamba kuna namna mbalimbali unazoweza kulinda mapato yako kwa kujitangaza moja kwa moja lakini kuangalia namna ambavyo unaongeza njia ya kuwafikia walengwa wako.
“Nimewasihi sana wafanye hivyo na kwa sasa wanawaza namna ya kufanya jambo hilo.”
Kwa sasa, mashabiki wanataka kupata haki ya kutazama kutoka kwenye vifurushi vyao vya BT Sports na Sky Sports wakati Amazon walionesha michezo 20 kwenye huduma yao ya Prime mwezi Desemba mwaka jana.
Kwa sasa, BBC inaonesha marudio ya gemu zote na Mechi ya Siku na Mechi ya Siku ya 2 siku ya Jumapili.
Uzoefu wote wa Premier League hautokuwa sawa bila ya wanaotoa sapoti lakini kuwa na sherehe ya mpira wa miguu bila ya gharama ya ziada itaenda mbali sana na kurahisisha upatikanaji wa uhondo maridadi kabisa.
Pamoja na ligi zingine kadha wa kadha za huko Ulaya, Premier League iliahirishwa kwa sababu ya mlipuko wa ugonjwa unaoendelea wa COVID-19.
Klabu za Premier League zilikutana mnamo siku ya Ijumaa wakiwa na lengo la kujadiliana namna ya kumaliza kampeni za msimu huu wa 2019/2020.
Klabu ziliwakilishwa kwa njia ya mawasiliano ya video na walikuwa wakionesha mipango mbalimbali juu ya namna nzuri ya kumaliza msimu na kuanza msimu mwingine na namna ambavyo kila timu zilizobakiwa na gemu tisa au kumi kuchezwa kati ya miezi ya Juni, Julai na Agosti mwaka huu.
Sky Sports wanaripoti kwamba tarehe ya jirani sana kwa Uingereza kuendeleza msimu wake huenda ikawa ni mwanzoni mwa mwezi wa Juni mwaka huu, Premier League haitolazimisha mipango yao iende mpaka pale serikali yao itakavyosema kuwa kwa sasa ni ruksa kufanya hivyo.


Sadick
Tunasubiri kwa hamu kuona mechi
Amani macha
Itakuwa vyema Sana ili mashabiki tupate burudani tulio ikosa kwa muda mrefu
Winfrida
Hii inapendeza watakuwa wamesadia na wanyonge
Nasra
Burudani itaendelea tunasubir
Salma
Hakika itakuwa safi sana
Samira
Burudani isiyo na kikomo kwa wapenzi wa soka la ulaya
John mwakalosi
Sasa yale makampuni yenyedhamana kama skysport ma BT sport si watakuwa wamepata hasara za mabilion ya pesa
Ester jackson
Hiyo siyo yakukosa lazima vingamuzi tuvilipie mapema tupate uhondo
Hopemwaikux
Mambo mazur karibia yaja
Mwanaidi
Burudani buree duuh hii ni noumaa sanaaaa
Theckla
Itakuwa vizuri
Hidaya Mohammed
Burudani mwanzo mwisho
Elika
Itakuwa vzr Sana wakionyesha bure
Warda candy
Bora tuonyeshwe tu mana
Dorophina
Tunaisubilia kwa mikono miwili
Furahav
Itakuwa poa sana
Emmy cleopa
Itakuwa vzr sana tupate burudani
Daniel
We cant wait for the Premier League with MeridianBet
Kenani
Mzigo wa luku upo wa kutosha
Rehema Dickson
kama skysport ma BT sport si watakuwa wamepata hasara za mabilion ya pesa
Issa
Ni vizuri waonyeshe wawape watu ladha
Povel
Gud news