Hivi umeshawahi kujiuliza ni mchezaji gani kutoka Uholanzi anafanya au alifanya poa sana ndani ya ligi kuu ya Uingereza, EPL? Bergkamp? Hasselbaink? Van Nistelrooy?
Kumekuwa na wachezaji waliobarikiwa ndani ya Premier League na unapotaja hao wachezzaji huwezi kukosa kuwataja wale waliopo huko wakitokea Uholanzi.
Mafanikio ya juu kisoka kufikiwa ndani ya EPL imejumuisha wachezaji kadha wa kadha kutokea Uholanzi. Jumla ya Waholanzi 133 wamecheza kandanda la kulipwa ndani ya Premier League tangu pale Hans Segers na Michel Vonk walipoingia kuchezea timu za Wimbledon na Manchester City katika ufunguzi wa msimu mpya wa Premier League miaka hiyo.
Baadhi wamekuwa watata sana uwanjani na wamekuwa wabunifu mno wakati wengine wakizipatia ulinzi mkubwa timu zao walizozitumikia kisoka.
Washambuliaji watatu kutokea Uholanzi wameshinda Golden Boot, ambapo akina Jimmy Floyd Hasselbaink na Robin van Persie wote hao wamenyakua tuzo hizo mara mbili na mwingine Ruud van Nistelrooy aliongoza katika takwimu ya wafungaji mabao wa msimu wa 2002/03 na pia akashinda tuzo ya Player of the Season.
Dennis Bergkamp anashikilia rekodi ya Premier League kwa kuongoza katika kutoa pasi za magoli kwenye mechi alizocheza, amesaidia upatikanaji wa magoli manne kwa Arsenal dhidi ya Leicester City mwezi Februari mwaka 1999.
Na katika upande mwingine wa uwanja, Edwin van der Sar ana rekodi kubwa sana ya kwenye upande wa clean sheets, anazo 14 jumla na ni kwa mfululizo kwa klabu ya soka ya Manchester United katika msimu wa 2008/09 wa EPL.
Ameweka clean sheets 132, hizo ni mara 86 zaidi ya kipa yeyote kutokea Uholanzi.
Angalia hapa namba zinazoongoza kwenye PL kwa wachezaji wa Uholanzi
| Mechi | Magoli | Pasi za Mabao | |||
| George Boateng | 384 | Robin van Persie | 144 | Dennis Bergkamp | 94 |
| Dennis Bergkamp | 315 | JF Hasselbaink | 127 | JF Hasselbaink | 58 |
| Edwin van der Sar | 313 | Ruud van Nistelrooy | 95 | Robin van Persie | 53 |
| JF Hasselbaink | 288 | Dennis Bergkamp | 87 | Dirk Kuyt | 27 |
| Mario Melchiot | 284 | Dirk Kuyt | 51 | Marc Overmars | 19 |
Van der Sar alifuata nyayo za mwenzake kutoka taifa moja, Jaap Stam, ambaye aliwika sana kwa klabu ya Man Utd kati ya miaka ya 1998 na 2001, akishinda taji kwenye misimu yake yote mitatu akiwa pale Old Trafford.
Kuna beki wa kati kutoka Uholanzi aliyewika na kuweka hatari sana katika misimu miwili iliyopita, huyu si mwingine bali ni Virgil van Dijk aliyeitumikia vyema sana klabu ya soka ya Liverpool na kufanikiwa kushinda tuzo ya Player of the Season msimu wa 2018/19.
Angalia takwimu hizo zinazovutia kwenye jedwali hapo juu kuweza kuona namna Waholanzi walivyofanya poa sana Uingereza. Kwako wewe unadhani ni nani anastahili kuwa mchezaji bora zaidi kutoka Uholanzi?


Sadick
Robin Van Persie was great striker
Amani macha
Mchezaji Bora alikuwa Ni van nistelrooy alikipiga Sana
Hopemwaikux
George boateng
Antony luseno
Bergkamp alikuwa hatar ktk assist
Mwanaidi
Namkubali sanaaaa huyo
Zainabu
Robin jamanii nikimuona natamani Mpira usiishe
John mwakalosi
Robin van persie alikuwa na kipindi au msimu mzuri hasa baada ya kupona majeraha yake ya mara kwa mara ila dennis bergkamp ni mchezaji bora wa muda wote kwenye premier
Ernest Kimeru
Salute kwa Dennis Bergkamp!!¡!
elika
Mario melchiot ni noumaaaa
Elika
Namkubali Sana Mario melchiot
Wahida
Van Nistelrooy Alifanya bia sana
Dorophina
Robin van persie yuko vizuri sana kuliko wengine
Furahav
Uholanzi wanatisha sana
Sylvester
Hao ni wachezaji moto wa Uholanzi..Asante Meridinbet kwa taarifa
Daniel
Legends
Kenani
Hn mpinzan hyo
Gabriel
Uholanzi wako vzur
Povel
Van persie mwamba