Washambuliaji Bora wa Nigeria Ndani ya Premier League

Nigeria ina vipaji vingi na imezalisha washambuliaji wakubwa sana kwa miaka mingi sasa. Baadhi ya washambuliaji hao wamejitengenezea majina yao kwenye ligi maarufu duniani, Premier League. Hata hivyo, ni nani amefunga mabao mengi na kuleta mabadiliko yaliyodumu? Hawa hapa ni washambuiaji 5 bora kutoka katika taifa la Nigeria ndani ya Premier League:

  1. Yakubu Ayiegbeni

Unapowafikiria washambuliaji wa Afrika wa muda wote, watu kama akina George Weah, Didier Drogba, na Samuel Eto’o wanakujia akilini mwako kwa haraka sana. Hata hivyo, mshambuliaji wa Nigeria, Yakubu Aiyegbeni anatakiwa kuwemo kati ya hao watatu. Mpaka leo hii hakuna mshambuliaji wa Nigeria ambaye amepachika mabao 95 ndani ya Premier League kama ambavyo mchezaji huyu amefanya.

Kiukweli, Waafrika ambao wamefanya poa sana na kufunga magoli zaidi ya hayo ni akina Drogba na Emmanuel Adebayor. Alianza kucheza ndani ya Premier League akiwa na klabu ya soka ya Portsmouth, kabla hajafanya vyema zaidi na kuwavutia akina Middlesbrough, Everton, na Blackburn. Kwenye gemu zake 252 ndani ya Premier League, Yakubu alifikisha idadi mara mbili ya mafanikio hayo katika misimu sita tofauti. Ingawa hajachezea timu kubwa huko Ulaya lakini alileta mchango mkubwa sana katika ligi hiyo maarufu duniani. Kwa hivyo hii inamfanya awe mchezaji bora wa Nigeria katika nafasi ya mshambuliaji ambaye anaingia katika 5 bora ya washambuliaji makini kutoka Nigeria kukipiga ndani ya ligi kuu ya Uingereza.

  1. Nwankwo Kanu

Bila shaka Kanu ni moja ya wachezaji wazuri sana kutokea barani Afrika. Ubora wa Kanu unajieleza wenyewe kwa hakika. Katika gemu zake 273 alizocheza ndani ya Premier League kwa klabu ya soka ya Arsenal, West Bromwich Albion na Portsmouth, Kanu amepiga mabao 54 jumla. Nani anaweza kusahau ile hatitriki yake bomba dhidi ya Chelsea, ambayo ikawanufaisha The Gunners wakatoka na ushindi mbele ya kuongozwa 2-0? Alishinda mataji kadhaa, mojawapo ni Champions League na mengine matatu ya Eredivisie, matatu ya FA, mawili ya Premier League. Ongezea hapo na mengine mawili ya African Player of the Year kwenye tuzo hizo. Kiujumla, anaweza kuwa ni moja kati ya wachezaji bomba wa Afrika kucheza ndani ya Premier League.

  1. Efan Ekoku

Mara ya mwisho Efan Ekoku alipoichezea Premier League ilikuwa ni mwaka 1999, hii inamaanisha kwamba hawezi kuwa anatambulika kwa mashabiki wengi wa soka kwa sasa. Hata hivyo, katika misimu yake saba alichangia upatikanaji wa mabao 52 katika gemu 158 alizozicheza uwanjani kwa klabu ya soka ya Norwich City na ile ya MK Dons. Pia, alikuwa ni sehemu muhimu sana ya kikosi cha Canaries kufikia nafasi ya tatu kwenye msimu wa 1993.

  1. Shola Ameobi

Ameobi alitumia muda wa miaka 14 akiwa ndani ya Newcastle United kwenye gemu zote za Premier League na zile za Championship, akajitwalia sifa ya ushujaa mkuu. Mshambuliaji huyu wa Nigeria alicheza jumla ya gemu 299 za ligi na kufunga jumla ya magoli 43. Kwenye gemu hizo zote ni mara nyingi alitokea benchi wakati akicheza nao. Ushujaa wake na jicho la kuona goli katika ligi kubwa ulimfanya awe mchezaji maridadi sana kikosini mwake. Pia, Ameobi aliwika mara mbili akiwa kama sub kwenye historia ya Premier League akiwa na gemu 142 za mtindo huo.

  1. Peter Odemwingie

Misimu sita kwenye Premier League ilileta jumla ya mabao 36 kwa mwanasoka machachari aitwaye Peter Odemwingie. Alivaa njuga zake kuchezea klabu za West Brom, Stoke City na Cardiff. Kuna vitu vinavyomtofautisha sana mshambuliaji Odemwingie wakati wa uwepo wake kwenye Premier League. Alishinda tuzo tatu za Player of the Month akimzidi Eden Hazard, Fernando Torres, Luis Suarez, Didier Drogba, na Ryan Giggs (wote hawa wanazo mbili tu). Odemwingie amefunga mabao 15 katika msimu wa 2010/2011, akamaliza akiwa wa 5 katika takwimu za wafungaji mabao kwenye ligi kuu ya Uingereza.

5 – Wafungaji mabao watano wa juu kwenye msimu wa 2010-11 Premier League:

20 | Dimitar Berbatov

20 | Carlos Tevez

18 | Robin van Persie

17 | Darren Bent

15 | Peter Odemwingie

Waliotajwa kwa ubora (Honourable mentions)

Obafemi Martins – magoli 28, Victor Anichebe – 26, Kelechi Iheanacho – 19, Odion Ighalo – 16. Iheanacho na Ighalo wanaongoza katika washambuliaji wa Nigeria waliocheza ndani ya Premier League mpaka muda huu.

19 Komentara

    Asante Meridian kwa habari hii nzuri

    Jibu

    Tunashukuru kwa taarifa

    Jibu

    Asantee Kwa taarifa meridianbet

    Jibu

    Tuko pamoja nanyi meridian

    Jibu

    Inamaana hawa ndio bora wa kuwai kutokea mpaka sasa kwenye ligi ya uingeleza

    Jibu

    Habari njema kwetu mashabiki hii

    Jibu

    Meridian mnanipa uhondo habar zote napata hapaa

    Jibu

    Asante kwa taharifa

    Jibu

    Ni vzr kwa wachezaji wa kiaftika kuonekana katika ligi kubwa kama hii kutoa hamasa kwa wengine kufanya vzr zaidi.

    Jibu

    Makala safi kabisa

    Jibu

    Tunashuru kwa taarifa meridian

    Jibu

    Nigeria Ni Moto kwa Africa kwa Wanasoka wa kihistoria!!!!

    Jibu

    asanteni kwa taarifa nzuri

    Jibu

    nigeria ni mfano wa kuigwa na afrika

    Jibu

    Waafrika wanatisha sana

    Jibu

    Shukurani sn meridianbet

    Jibu

    Nigeria ni zao la vipaji Africa

    Jibu

    Yakubu Ayiegbeni
    huyu jamaa alikuwa hatari sana pale Blackburn rovers enzi hizo

    Jibu

    Waafrika wana vipaji

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.