Mchezaji kinda wa Tenisi, Emma Raducanu alionyesha mchezo wake katika ushindi dhidi ya Caroline Garcia huko Indian Wells baada ya kurejea kutoka kwenye majeraha.
Raducanu alipata jeraha la mguu katika mechi za nchini Mexico wiki mbili na nusu zilizopita na alihofia kwamba angekosa BNP Paribas Open huko Indian Wells, mojawapo ya mashindano makubwa zaidi kwenye Ziara ya WTA.
Lakini alifaulu mtihani wa utimamu wa mwili kwa kuchelewa kuchukua nafasi yake katika droo kubwa na alitumia vyema fursa yake kwa uchezaji wa kuvutia kumshinda Garcia kwa seti 6-1 3-6 6-1.

“Nimefurahi sana kupata ushindi wangu wa kwanza hapa jangwani na natumaini nitarejea hapa kwa miaka mingi zaidi. Nadhani kiwango cha tenisi kilikuwa cha juu sana leo kwa hivyo ina maana kubwa kwangu kwasababu yeyote angeweza kushinda,” Raducanu alisema..
Emma Raducanu atakutana na Petra Martic katika raundi ya tatu Jumapili baada ya Mcroatia huyo kumuondoa Tamara Zidansek anayeshika nafasi ya 19 duniani kwa 7-5 7-6 (8-6).
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


