Ukimuangalia kwa haraka haraka, utamuona ni mtu mpole tu. Lakini, Ralf Rangnick ni mtu complex na, anamisimamo migumu kuliko anavyoonekana.
Pengine wapo waliombeza wakati anatajwa kuchukua nafasi ya Michael Carrick kama kocha wa muda, hawakumdhania kama mtu atakayeweza kuongoza kundi la wachezaji ambao wamezoeleka kuwa wakubwa kuliko kocha. Kwa Ralf, wamegonga mwamba.
Sio Paul Pogba, Cristiano Ronaldo, Bruno Fernandes, Marcus Rashford, Jesse Lingard, Marcus Rashford, Edinson Cavani wala Anthony Martial ambaye ameweza kumtikisa Rangnick. Hii ni kutokana na uwezo wake wa kuonesha msimamo bila kujali ukubwa wa jina lako ndani na nje ya uwanja.
Ralf Rangnick ni mtu wa tofauti kabisa na Ole Gunnar Solskjaer. Mjerumani huyu, hawezi kuwabeba wachezaji hasa anapokuwa kwenye vyombo vya habari. Wazungu wanasema “he speaks his mind” kwa lugha nyepesi, hakwepeshi maneno, anasema kile anachokiamini na kukiona.
Kwa Ralf, ukifanya vizuri atakusifia na, ukifanya vibaya atakusema vilevile. Lengo lake sio kukufanya ujisikie vibaya na usiye na thamani, la hasha! Siku zote anaonesha msimamo wake wa kutaka kila mchezaji kuongeza juhudi na kuiweka timu mbele kuliko mafanikio binafsi.

Hasiti kumueka mchezaji yeyote benchi kama kufanya hivyo kutaleta matokeo chanya kwenye timu yake uwanjani. Wachezaji nyota wa Man United wote wanaonja joto ya jiwe kwa maisha chini ya Rangnick, hakika, hii ni roho na akili thabiti ya kijerumani.
Wakati huu ambao CR7, Rashy na Pogba wanahusishwa na kuondoka United, Ralf amekua akitoa msimamo ule ule kwa wachezaji wote. Yeyote anayeona hawezi kuendelea kuwa hapa na pengine anataka kuondoka, milango ipo wazi. Dirisha la usajili likifunguliwa, kila mmoja ananafasi ya kuamua njia anayotaka kuichukua.
Japokuwa, katika kufanikisha hilo, Ralf Rangnick anasisitiza, matakwa ya klabu lazima yafikiwe ili usajili wowote uwezekane. Kwa maana hiyo, mchezaji ataamua anachotaka lakini, klabu inanguvu zaidi ya mchezaji na hivyo, pande zote mbili lazima ziafikiane na sio kufanya maamuzi ya pande moja.
Sambamba na hilo, Ralf Rangnick haamini katika kumbebesha kocha mzigo wa wachezaji wanaocheza chini ya kiwango. Kwake anaamini, kiwango cha mchezaji kinaanzia kwa mchezaji mwenyewe, kocha anaongezea tu. Na hivyo, juhudi binafsi za mchezaji ndio chachu ya kuongeza/kupunguza kiwango chake.

Hili limejidhihirisha kwa Jadon Sancho na Anthony Elanga ambao, wote hawakua kwenye kiwango bora kabla ya ujio wa Ralf Rangnick, lakini, aliwapa nafasi ya kuonesha uwezo na juhudi zao mazoezini na uwanjani. Sasa hivi, hawa ndio wachezaji wanaoibeba United kwa sehemu kubwa.
Akili na uwezo wa kijerumani unaiongoza Manchester United kwa sasa. Kazi kwao wachezaji wa klabu hiyo kuendana na misimamo konki ya kocha wao.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


