Usiku wa jana akaunti ya twitter ya Rashford ilionekana ikijibu moja ya tweet iliyouliza kuhusu Sancho kutua United, lakini Mwingereza huyo amekanusha kauli kuhusu taarifa za Sancho kutua United.
Kwa kipindi kirefu sasa Sancho amekuwa akihusishwa kujiunga na Manchester United, huku Dortmund ikionekana kutaka dau kubwa na sasa inaonekana dili hilo litakamilika hivi karibuni.
Rashford alipinga kujibu tweet ya shabiki mmoja kwa kile alichodai kuwa akaunti yake ya Twitter ilikuwa imedukuliwa kwa masaa kadhaa na hapo ndipo tweet hiyo ilijibiwa.
Dortmund wanaonekana kukubali dili la sasa la Pauni milion 77 ambayo ni sawa na dola milioni 100, Manchester United tayari wameshakubaliana na Sancho na sasa inasubiriwa tu winga huyo kutua United kucheza na Rashford.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

