Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford amesema ana furaha na kocha wasasa wa klabu hiyo bwana Eric Ten Haag.rashfordKocha Ten Haag ambaye amechukua nafasi ya mwalimu aliepita klabuni hapo Ralf Rangnick ambaye pia alikua kwa muda baada ya kuchukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer.

Tangu kuja kwa kocha huyo klabuni hapo imeonekana kuleta mabadiliko kwenye timu hiyo kuanzia kwa wachezaji kitu ambacho kimewafanya wachezaji wa timu hiyo kuvutiwa na mwalimu huyo akiwemo Marcus Rashford.rashfordTen Haag ambaye alionekana kuanza vibaya katika timu hiyo baada kupokea vipigo viwili katika michezo yake ya kwanza lakini amefanikiwa kuibadili timu hiyo. Na sasa klabu hiyo inafanya vizuri kwa kiwango fulani.

Rashford aliulizwa na waandishi wa habari namna gani anamzungumzia kocha huyo na kusema ni furaha kufanya naye kazi, na ni ngumu pia kufanya nae kazi lakini wanafurahia kucheza soka bora zaidi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa