Rashford Mchezaji Bora Mwezi Febuari Epl

Mshambualiaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford amechaguliwa kua mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza kwa mwezi Febuari baada ya kutwaa tuzo ya klabu wiki moja iliyopita.

Marcus Rashford amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya pili mfululizo baada ya kutwaa tuzo hiyo mwezi Januari, Mchezaji huyo pia amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa klabu yake kwa mwezi wa pili mfululizo.RashfordStaa huyo wa kimataifa wa Uingereza amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji kama Bukayo Saka, Emerson Royal,Benard Leno, Olie Watkins, na Kelechi Ihenacho mchezaji huyo akiibuka kidedea baada ya kucheza kwa kiwango cha juu kwa mwezi Febuari.

Marcus Rashford amekua kwenye kiwango bora ndani ya mwezi wa pili akifanikiwa kucheza michezo minne na kufunga mabao matano ya ligi kuu ya Uingereza, Huku klabu yake ya Manchester United ikifanikiwa kushinda michezo mitatu na kusuluhu mchezo mmoja na kuvuna alama 10.RashfordMchezaji Rashford amekua kwenye kiwango cha hali ya juu tangu kumalizika ka michuano ya kombe la dunia na kufanikiwa kua mchezaji aliefunga magoli mengi baada ya michuano ya kombe la dunia, Kiwango kilichomuwezesha kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ligi kuu ya Uingereza mara mbili mfululizo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.