Real Madrid wamefanikiwa kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa jumla ya magoli 3-2 baada ya mshambuliaji Karim Benzema kufunga hat-trick yake kipindi cha pili na kuisaidia klabu yake kusonga mbele.

Kylian Mbappe alianza kufunga na kuongeza faida ya PSG kuwa mbele kwa magoli 2-0 baada ya kumalizia pasi safi kutoka kwa msambuliaji mwenzake Neymar katika dakika ya 39 ya mchezo.
Katika kipindi cha kwanza PSG walimiliki mchezo uwanjani Santiago Bernabeu kabla ya Real Madrid kumlazimisha Gianluigi Donnarumma kufanya makosa na Benzema kumalizia pasi ya Vinicius Jr.
Benzema, ambaye alikua mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga hat-trick ya Ligi ya Mabingwa Jana usiku, anampita Alfredo Di Stefano kama mfungaji wa tatu kwa ufungaji Real Madrid kwa mabao 309.
“Tulipoteza katika mechi ya kwanza, tulikuwa tumepoteza wakati wa mapumziko… Ilikuwa ngumu sana, lakini hii ni mechi ya Ligi ya Mabingwa na sisi ni Real Madrid,” Benzema, nahodha wa washindi mara 13 wa Ligi ya Mabingwa, alisema baada ya mchezo.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


